Jeshi la Sudani laiweka tena kwenye himaya yake ikulu ya rais mjini Khartoum

Takriban miaka miwili baada ya kutekwa kwake na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ikulu ya rais mjini Khartoum imerejea katika udhibiti wa jeshi la Sudani siku ya Ijumaa. Mzozo kati ya Jenerali Abdel Fattah Abelrahman Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdane Daglo unaikumba nchi hiyo na tayari umesababisha makumi kwa maelfu ya watu kuuawa.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Nchini Sudani, wanajeshi wa jeshi la serikali ya Sudan waiweka tena kwenye himaya yake ikulu ya rais siku ya Ijumaa, Machi 21, baada ya kutekwa na wanamgambo hao karibu miaka miwili iliyopita, chanzo cha kijeshi kimeliambia shirika la habari la AFP.

“Vikosi vyetu vimevamia ikulu (ya rais) na kuchukua udhibiti wake baada ya kuwaangamiza mabaki ya wanamgambo,” chanzo kimesema kwa sharti la kutotajwa jina, kikimaanisha Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), kundi la wanamgambo ambalo limekuwa likishikilia ikulu ya rais huko Khartoum tangu kuzuka kwa vita na jeshi mnamo mwezi wa Aprili 2023 Habari hii imethibitishwa na shirika la habari la REUTERS.

Jeshi linaendesha shughuli za msako katika maeneo yanayozunguka ikulu kuwasaka wapiganaji wa FSR, kulingana na vyanzo vya shirika hilo la habari la Uingereza.

“Vita vya kudhibiti kabisa ikulu bado havijaisha,” FSR ilitangaza asubuhi ya leo katika taarifa iliyotolewa kwenye Telegram, na kuongeza kwamba wapiganaji wake “wameua zaidi ya maadui 89 na kuharibu magari kadhaa ya kijeshi.”

Chanzo cha habari cha jeshi la Sudani pia kimesema kuwa waandishi watatu waliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye ikulu ya rais, saa chache baada ya jeshi kuchukuwa tena udhibiti makao makuu ya mamlaka.

Waandishi hao walikuwa wakitumikia televisheni ya taifa ya Sudani wakati RSF ilipolenga Ikulu ya rais kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya njia moja, chanzo kimeliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

Jeshi la Sudani latekamaeneo kadhaa

Jeshi la Sudani limepiga hatua katika wiki za hivi karibuni dhidi ya RSF, ambayo imedhibiti sehemu kubwa ya magharibi mwa Sudani tangu kuanza kwa vita na inajaribu kuimarisha udhibiti wake katika jimbo la Darfur.

Mgogoro wa kuwania madaraka kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah Abdelrahman Burhan na makamu wake wa zamani, Mohamed Hamdane Daglo, kamanda wa RSF, tayari umesababisha makumi ya maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni 12kutoroka makazi yao.

Katika eneo la mji mkuu wa Khartoum pekee, watu wasiopungua milioni 3.5, zaidi ya nusu ya wakazi wa kabla ya vita, wamekimbia makazi yao.

Mzozo huo umegawanya nchi hiyo pande mbili, huku jeshi likidhibiti kaskazini na mashariki, na FSR ikidhibiti sehemu kubwa ya magharibi na kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *