Jeshi la Sudan: Tumevunja mzingiro wa RSF Khartoum

Jeshi la Sudan limetangaza habari ya kufanikiwa kuvunja ‘mzingiro’ uliowekwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya Kamandi Kuu ya jeshi hilo katikati mwa Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.