Jeshi la Sudan na RSF wapigana kuhusu kinu cha kusafisha mafuta kaskazini mwa Khartoum

Mapigano makali yaliendelea kwa siku ya pili jana Alhamisi kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo hasimu wa jeshi hiyo yaani Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) karibu na kinu cha kusafisha mafuta kaskazini mwa mji mkuu, Khartoum.