
Jeshi hilo limesema kama sehemu ya mipango yake ya ulinzi, limeamua kuwaondoa wanajeshi wake mpakani.
Jeshi la Sudan linalopambana dhidi ya RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, linawatuhumu wanamgambo hao na vikosi vya Haftar kutumia eneo la mpakani kama njia ya kupitisha silaha. Eneo hilo lipo karibu la mji wa Al Fashir moja ya ngome za vita vinavyoendelea.
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Sudan vyaanza kutekelezwa
Sudan inadai Umoja wa Falme za kiarabu UAE, inayomuunga mkono kamanda wa kijeshi Mashariki mwa libya Khalifa Haftar kuwa nyuma ya mipango ya kupitisha silaha, madai ambayo UAE inayakanusha vikali. Misri mmoja wa washirika wakubwa wa jeshi la Sudan pia inamuunga mkono Haftar.