Jeshi la Sudan ladhibiti kikamilifu kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini humo

Jeshi la Sudan limeeleza kuwa limechukua udhibiti kamili wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha al Jaili karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum huku gavana mmoja wa nchi hiyo akiripoti kuuawa watu zaidi ya 70 katika shambulio la droni lililotekelezwa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko al Fasher magharibi mwa Sudan.