Jeshi la Sudan lachukua udhibiti wa kituo kikuu cha wanamgambo wa Rapid Support Forces

Jeshi la Sudan limetangaza kudhibiti kikamilifu mji wa Jiad, kituo kikuu cha wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) karibu na Khartoum. Mafanikio hayo yanatambuliwa kuwa ni hatua muhimu na ya kimkakati katika njia ya kulinda mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.