Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia Daud Delim (49) mkazi wa Mbagala ‘A’ wilayani Igunga kwa tuhuma za kujiita Mkuu wa Kituo cha Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari amesema wamemkamata Daudi kwa madai ya kufanya mahojiano yaliyosambaa katika mitandao ya kijamii yenye lengo la upotoshaji na kueleza kuwa hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.
#Azamnewsupdates
✍Juma Kapipi
Mhariri | @official_jennifersumi