Jeshi la Polisi lawashikilia vijana zaidi ya 100 kwa biashara ya upatu

Kibaha. Zaidi ya Vijanana na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu nchini.

Vijana hao wasichana na wavulana ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 2,2 wamekutwa mjini Mlandizi, Mkoa wa Pwani ambapo inadaiwa kuwa wamekuwa wakitumia njia inayoendana na upatu ili kujiingizia kipato.

Akizungumza akiwa eneo la tukio Februari 15, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salimu Morcase amesema, wanaendelea kuwafanyia mahojiano kisha hatua zingine zitafuata.

“Hawa vijana wanatoka mikoa mbalimbali na maelezo ya awali yanaonyesha kuwa wanajihusisha na shughuli zinazokaribiana na mambo ya upatu, jambo ambalo ni kinyume na sheria,” amesema.

Kamanda Morcase amesema kuwa shughuli wanazojihusisha nazo vijana hao, hazina mwelekeo mzuri na zinaweza kuwaingiza kwenye vishawishi vinavyoweza kuharibu mfumo mzima wa maisha yao,” amesema.

Mmoja wa vijana hao akizungumza kwa sharti la kutotaja majina yake, amesema wamefika maeneo hayo kwa nyakati tofauti na kila anayefika huita wengine.

“Mimi natoka Mkoa wa Lindi nimekuja hapa mwezi wa kwanza nilipigiwa simu na mwenzangu akaniambia nije na mtaji wa kulipia bidhaa ninayotaka na nitapata faida pindi nitakapoleta mtu mwingine tena,” amesema.

Amesema kuwa baada ya kufika alilipia bidhaa mtandaoni na hivi sasa anaendelea kutafuta watu wa kuwaunganisha, ndipo aanze kupata faida.

Kijana mwingine aliyesema anatoka Mkoa wa Manyara anaeleza kuwa tangu afike eneo hilo anatimiza miezi minne sasa.

“Baada ya kufika nilichagua bidhaa mtandaoni nikalipa kisha nikatafuta watu wawili, baada ya kuwaunganisha nimeshapata faida ya Sh200,000.”