Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lataka wananchi wawe watulivu, waasi wasonga mbele

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Jumanne lilitoa mwito kwa raia kuwa watulivu kutokana na kusonga mbele waasi wa M23 hivi karibuni katika jimbo la Kivu Kaskazini la mashariki mwa nchi hiyo.