Jeshi la Israeli latumwa kusini mwa Syria kuunga mkono Druze, UN yataka mashambulizi yakome

Jeshi la Israeli limetangaza siku ya Jumamosi, Mei 3, kwamba limetumwa kusini mwa Syria, ambako limesema liko tayari kuingilia kati kulinda vijiji vya jamii ya walio wachache ya Druze kufuatia mapigano makali yaliyotokea mapema wiki hii kati ya vikosi vya serikali na waumini hawa walio wachache wa dini hii ndogo.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israeli linasema “limetumwa kusini mwa Syria” na kuongeza kuwa “liko tayari kuzuia kuingia kwa vikosi vya maadui katika eneo la vijiji vya Druze,” anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. Hii ni licha ya shutuma za Umoja wa Mataifa na maonyo ya kimataifa kuhusu hatari ya kuzorota kwa usalama nchini Syria. Taarifa hiyo ya kijeshi haikutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanajeshi wa Israeli nchini Syria au ukubwa wa wanajeshi hao. Kinachoonekana wazi ni kwamba Israeli inajiandaa kwa maendeleo zaidi katika eneo hili.

Katika usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, zaidi ya mashambulio ishirini ya Israeli yalilenga maeneo ya kijeshi kote Syria, “machafuko zaidi” mwaka huu kulingana na Shirika la Haki za Binadamu la Syria. Israel ilitangaza kuwa ilifanya shambulizi alfajiri ya Jumamosi kama onyo dhidi ya shambulio lolote dhidi ya walio wachache kutoka jamii ya Druze nchini Syria, kufuatia ghasia za kimadhehebu mapema wiki hii kati ya makundi yenye silaha yenye uhusiano na serikali ya Syria na wapiganaji wa Druze ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 100, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (SOHR). Shirika la habari la serikali ya Syria SANA limetangaza kuwa “raia” mmoja ameuawa katika mashambulizi hayo ya usiku.

Jeshi liliongeza kuwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, “raia watano kutoka jamii ya Druze kutoka Syria walihamishwa ili kupata matibabu nchini Israeli […] baada ya kujeruhiwa katika eneo la Syria.” Kwa mujibu wa jeshi la Israeli, watu kumi na watano kutoka jamii hii ya walio wachache chini Syria pia wamelazwa katika hospitali ya Safed kwa matibabu baada ya kujeruhiwa nchini Syria tangu siku ya Jumatano.

Siku ya Ijumaa, shambulio la onyo llifanyika katika maeneo ya karibu ya ikulu ya rais katika kile kilichokusudiwa kuwa ujumbe kwa utawala wa Syria. Ofisi ya rais wa Syria imelaani hatua hiyo ya pili kama “hatari ya kuongezeka kwa uhasama.”

UN yaitaka Israeli kusitisha mashambulizi “mara moja”

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Geir Pedersen ametoa wito kwa Israel siku ya Jumamosi “kusitisha mara moja” mashambulizi yake na “kukomesha kuhatarisha raia wa Syria na kuheshimu sheria za kimataifa.” “Ninalaani vikali kitendo cha Israeli kuendelea na kuongezeka kwa ukiukaji wa uhuru wa Syria, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mengi ya anga huko Damascus na miji mingine,” amesema katika taarifa yake.

Kulingana na afisa kutoka jamii ya Druze katika mkoa wa Sweida, “hakujawa na kutumwa kwa wanajeshi wa Israeli” katika eneo hili, ngome ya walio wachache wa Druze kusini mwa Syria. “Uwepo wao utakuwa mdogo katika jimbo la Quneitra,” magharibi zaidi, “ambapo waliweka ngome zao baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar Al-Assad” mwezi Desemba, ameliambia shirika la habari la AFP.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli, kwa upande wake, imebainisha kuwa Israeli haitaruhusu kutumwa kwa vikosi kusini mwa Damascus au vitisho vyovyote kwa jamii ya Druze. Benjamin Netanyahu alikutana na kiongozi wa kiroho wa jamii ya Druze nchini Israeli, Sheikh Muwaffaq Tarif.

Baada ya Assad kuangushwaa kutoka madarakani, jeshi la Israeli lilitangaza kwamba lilitumwa katika eneo hili, ambalo kinadharia halina jeshi upande wa mashariki wa mstari wa usitishwaji mapigano wa mwaka 1973 kati ya Syria na Israeli kwenye Golan ya Syria, ili kuzuia hatua zozote za uhasama kutoka kwa nchi jirani. Israeli imeikalia kwa mabavu sehemu ya Milima ya Golan ya Syria tangu mwaka 1967, ambayo ilitwaanyakuwa mwaka 1981. Nchi hiyo inatilia shaka mamlaka mpya ya Damascus, ambayo ni sehemu ya vuguvugu la kijihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *