Jeshi la Israel linaendelea kuteketeza roho za watu wasio na hatia Ghaza na Lebanon

Katika siku ya 416 ya vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni unaendeleza mashambulizi ya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo na vilevile wananchi wa maeneo mbalimbali ya Lebanon.

Vikosi vya jeshi la utawala haramu wa Israel vimetoa amri mpya ya kuhama katika mji wa Shujayea wa Ghaza, na kupelekea mamia ya Wapalestina kulazimika kulikimbia eneo hilo baada ya hujuma za kinyama za jeshi hilo la kizayuni kuwaua shahidi watu 38.

Hayo yanajiri wakati idadi ya watu waliouawa shahidi kutokana na shambulio la jeshi la utawala wa Kizayuni katikati mwa mji mkuu wa Lebanon Beirut ikiongezeka hadi 20, huku waokoaji wakiendelea kuchimbua vifusi kuwatafuta manusura. Watu wengine 66 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Tangu Oktoba 7, 2023 hadi sasa, mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanya na jeshi la utawala wa Kizayunil huko Ghaza yameshaua shahidi Wapalestina wasiopungua 44,176 na kujeruhi 104,473. 

Nchini Lebanon, watu wapatao 3,670 wameuawa shahidi na 15,413 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel tangu vilipoanza vita dhidi ya Ghaza…/