Jeshi la Israel lawaua kwa kuwapiga risasi watoto wa miaka 12 na 13 Wapalestina Ukingo wa Magharibi

Watoto wawili wa Kipalestina wenye umri wa miaka 12 na 13 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa mfululizo wa mashambulizi mengi yaliyofanywa na jeshi hilo usiku kucha wa kuamkia leo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yakijumuisha maeneo ya Tulkarem, Jenin na Nablus.