Jeshi la Israel launda kifaa cha AI cha kuwajasisi Wapalestina

Uchunguzi mpya umefichua kuwa, kitengo cha ujasusi wa kielektroniki cha jeshi la Israel cha 8200 kimetumia mkusanyiko mkubwa wa mawasiliano yaliyonaswa kutengeneza chombo cha kijasusi cha Akili Mnemba (AI) ambacho modeli yake inashabihiana na ChatGPT, kwa lengo la kuwachunguza na kuwafanyia ujasusi wananchi wa Palestina.