
Jeshi la Israel limethibitisha kutekeleza shambulio katika kile limesema ni hospitali ambayo ilikuwa inatoa hifadhi kwa magaidi wakati wa oparesheni zake katika Ukanda wa Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hamas inasema wanahabari aliuuawa katika shambulio hilo wakati akipokea matibabu baada yake kujeruhiwa kwenye shambulio jengine la Israel mwezi uliopita.
Shambulio hilo limejiri baada ya kuwepo kwa usitishaji mfupi wa mapigano kuruhusu kuachiwa kwa mateka mwenye uraia wa Marekani aliyekuwa anazuiliwa Gaza.
Kupitia mtandao wake wa Telegram jeshi la Israel limesema magaidi wa Hamas walikuwa wanaitumia hospitali hiyo ya Nasser katika eneo la Khan Yunis kusini mwa Gaza kuendeleza shughuli zao.
“Jengo hilo lilikuwa linatumika na magaidi kupanga na kutekeleza mashambulio ya kigaidi dhidi ya raia wa Israel na wanajeshi wa IDF,” Ilisema taarifa ya jeshi.
Kulingana na Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza, watu wawili waliuawa kwenye shambulio hilo wakati wengine wakijeruhiwa.
Vyombo vya habari vinavyomilikuwa na Hamas navyo vimesema mwanahabari imesema Hassan Aslih aliuuawa kwenye shambulio hilo.