Jeshi la Israel laendelea kukalia maeneo ya ardhi ya Lebanon licha ya muhula wa kuondoka kumalizika

Muhula wa mwisho uliokuwa umetolewa kwa askari wote wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuondoka kusini mwa Lebanon chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya utawala huo na harakati ya Hizbullah ulimalizika leo Jumanne, huku Israel ikitangaza kuwa itaendelea kubaki katika “maeneo matano ya kimkakati” ya ardhi ya nchi hiyo.