Jenerali wa Iran: Mazishi ya viongozi wa Muqawama ni hamasa ya kudumu Asia Magharibi na Lebanon

Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Baqeri, amesema kuwa mazishi na shughuli za kuaga mashujaa wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon yamekuwa tukio la hamasa ya kihistoria lisilosahaulika katika historia ya eneo la Asia Magharibi na Lebanon.