‘Jehanamu halisi’: Wanawake wa Sudan wanavyokabiliwa na ubakaji na unyanyasaji nchini Libya

“Tunaishi kwa hofu,”Layla anasema kwa njia ya simu kwa sauti ya kunong’oneza ili mtu asimsikie . Alitoroka Sudan na mumewe na watoto sita mapema mwaka jana kutafuta usalama na sasa yuko Libya.