Jean Baleke anukia AmaZulu FC

KUNA uwezekano mkubwa wa straika wa zamani wa Simba na Yanga, Jean Baleke akajiunga na AmaZulu FC ya Afrika Kusini, baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina yake na  uongozi wa timu hiyo kuhitaji huduma yake.

Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kilichobakia ni Baleke kusaini mkataba huo, kwani kila kitu kimekamilia kwa  asilimia kubwa endapo kama hakutatokea jambo lingine la kufanya dili hilo lisitiki.

“Kuna asilimia kubwa Baleke akasaini Amazulu FC kwa sababu makubaliano kati yake na uongozi wa timu hiyo yalikuwa yamekwenda vizuri, kilichokuwa kimabakia ni kusaini mkataba,” kimesema chanzo hicho na kuongeza:

“Nje na Amazulu FC kulikuwepo na  timu nyingine ambazo zilikuwa zinawinda saini yake za ndani na nje, kikubwa alichokiangalia ni maslahi yake.”

Kwa muda aliocheza Simba alifunga manane akiwa amesajiliwa wakati wa dirisha dogo la msimu wa 2022/23 (manane), akaondoka lile dogo la 2023/24 kwenda kujiunga na Al-Ittihad kisha akajiunga Yanga ambayo imeachana nayo msimu huu akiwa amefunga bao moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *