Je, ulimwengu unapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu virusi vipya HMPV?

HMPV kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mtu aliyeambukizwa kwenda kwa wengine kupitia kukohoa na kupiga chafya. Vinaweza pia kusambazwa kupitia mgusano wa karibu, kama vile kugusa au kushikana mikono, au kugusa vitu au maeneo vilivyo na virusi na kisha kugusa mdomo, pua au macho.
Virusi hivi husambaa zaidi katika miezi ya msimu wa baridi ambapo watu hukaa ndani ya majumba.