Je, ni nani aliyehusika na vifo vya wanandoa wafanyabiashara waliokuwa wakiishi pamoja eneo la Bonyokwa, Wilaya ya Ilala? Swali hilo limeendelea kuwahangaisha wakazi wa eneo hilo kufuatia tukio la kusikitisha la kuuawa kwa Antoni Hilary Ngabori na Anna Amir Juma.
Ingawa bado haijafahamika nini hasa kilitokea, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeanza uchunguzi rasmi huku matumaini ya wengi yakiwa ni kupata majibu ya nani aliyehusika na tukio hilo la kikatili.
#azamnewsupdates
✍@joempangala
Mhariri|@official_jennifersumi