Je, Morocco yaweza kumrejesha Macky Sall nchini Senegal ili afunguliwa mashitaka?

Nchini Senegal, Wabunge wanatarajiwa kupiga kura katika kikao cha mashauriano leo Jumanne Machi 11 kuhusu mswada ambao utamuwezesha Rais wa Jamhuri kuidhinisha makubaliano ya usaidizi na uhamisho wa wafungwa wa Senegal walioko Morocco kupelekwa katika nchi yao ya asili na kinyume chake. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Wakati serikali imetangaza kwamba Rais wa zamani Macky Sall, ambaye amekuwa akiishi Morocco tangu kuondoka madarakani, “atakabiliwa na mkono wa sheria”, je, makubaliano haya yanaweza kutumika katika muktadha wa uwezekano wa mashtaka dhidi yake?

Mkataba kati ya Morocco na Senega uliyotiwa saini zaidi ya miaka ishirini iliyopita mnamo Desemba 2004,  haujawahi kuidhinishwa. Kiuhalisia, mkataba huu unapaswa kuwezesha mtu aliyetiwa hatiani katika mojawapo ya nchi hizo mbili kutumikia kifungo chake katika nchi yake ya asili, huku akinufaika na misaada ya kibalozi na ya kibinadamu.

Kulingana na seti ya vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi ya habari ya serikali kwa hfla hiyo, Wasenegali 299 wanaozuiliwa kwa sasa nchini Morocco kwa uhamiaji haramu, uuzaji wa madawa ya kulevya au kushirikiana na kundi la wahalifu miongoni mwa mengine, wanaweza, kutokana na makubaliano haya, kunufaika kutokana na kurejea Senegal. 38  inaaminika kwamba tayari wameomba kurejshwa nchini Senegal. Kwa sababu, ijapokuwa makubaliano ya kurejeshwa nchini yamekuwepo kati ya nchi hizo mbili tangu mwaka 1967, hakuna kilichopangwa kwa ajili ya usaidizi na uhamisho wa watu waliohukumiwa.

“Kazi bure”

Kwenye karatasi, hakuna uhusiano kati ya makubaliano haya ya kuhamisha wafungwa kutoka Morocco kwenda Senegal na kesi ya rais wa zamani Macky Sall. Lakini, wakati serikali inaahidi kwamba “atakabiliana na mkono wa sheria”, muda wa kupitishwa kwa mkataba huu wa zamani unatia shaka. Je, unaweza kusaidia kumrudisha rais huyo wa zamani iwapo atafunguliwa mashitaka au kukutwa na hatia?

“Kazi bure,” wamejibu wajumbe kadhaa wa serikali. Kulingana na mwangalizi wa mashirika ya kiraia, huu ni “mchezo wa kisiasa” kwa sababu kumtuma rais wa zamani ni jambo gumu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *