Jamii ya Tuareg yawasilisha kesi mahakamani dhidi ya Mali na Burkina Faso

Muungano wa jamii ya Tuareg, nchini Mali na Burkina Faso, umewasilisha kesi katika mahakama ya ICC, dhidi jeshi la mataifa hayo kuhusika kwenye uhalifu wa kivita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Muungano huo unatuhumu jeshi la Mali na Burkina Faso, kwa kuhusika kwa uhalifu wa kivita ikiwemo, mauwaji, utekaji, mateso na kupora mali ya raia, visa vilivyofanyika tangu mwaka 2022.

Kadhalika muungano huo unatumuhu utawala wa kijeshi katika mataifa hayo kwa kutafuta msaada wa mamluki wa Urusi, Africa Corps, ambao pia wametajwa kuhusika katika mauwaji ya raia zaidi ya 60 mwezi April katika eneo la kwala.

Tayari ICC ilikuwa inaendesha uchuguzi wa uhalifu wa kivita nchini Mali, uliofanyika eneo la Timbuktu mwaka 2012, ila kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo kumechangia uchuguzi huo kusitishwa.

ICC sasa inatarajiwa kutoa taarifa kuhusiana na kesi hiyo katika harakati za kuhakikisha waathiriwa wanapata haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *