Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yataka uchunguzi wa ukiukaji wa haki katika mji wa Goma

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itawasilisha hoja katika Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa kutaka uchunguzi wa kile ilichokiita “ukiukwaji mkubwa” wa haki katika mji wa Goma.