Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda zimetia saini mpango wa usalama wa mashariki mwa DRC ambao hatimaye unaweza kuondolewa kwa maelfu ya wanajeshi ambao Kigali inaaminika kuwapeleka katika eneo lenye machafuko.
Tangazo kuhusu makubaliano hayo lilitolewa na serikali ya Angola, ambayo ni mpatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) wa mzozo wa mashariki mwa DR Congo, lakini uthibitisho rasmi bado haujatolewa na nchi hizo mbili.
Tovuti binafsi ya habari ya Actualite imesema mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda walifikia makubaliano mjini Luanda juu ya “mpango uliooanishwa” wa “kuondoa” kundi la waasi wa Kihutu lililoundwa na wahusika wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, FDLR.
Ilisema kuwa mpango wa kina utafanyiwa kazi katika mazungumzo yajayo kati ya pande hizo mbili.
Majaribio ya hapo awali ya kukamilisha makubaliano hayo, ambayo maelezo yake yalitolewa wakati wa mazungumzo ya siri mwezi Agosti kati ya wakuu wa kijasusi wa nchi hizo mbili, yalishindwa kutekelezwa huku kila upande ukitaka upande mwingine utimize wajibu wake kwanza.
Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wa ndani mashariki mwa

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Duru mbalimbali katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini zimeripoti kuhusiana na wimbi hilo jipya la wakimbizi.
Mwezi Januari mwaka huu Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilitangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.