Jaji mkuu wa Mahakama ya Juu amshtumu Trump baada ya wito wake wa kumfuta kazi jaji

Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Marekani John Roberts, siku ya Jumanne, Machi 18, amemkosoa rais wa Marekani, ambaye hapo awali alimshambulia jaji kwenye mitandao ya kijamii kwa kutaka kesi ya kumfungulia mashtaka ichukuliwe. Kauli adimu kutoka kwa mtu anayesimamia chombo cha juu zaidi cha mahakama nchini. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Marekani, Edward Maille

Huu ni msimamo adimu sana. “Kushtakiwa sio jibu linalofaa kwa kutokubaliana juu ya uamuzi wa mahakama,” alisema Jaji wa kihafidhina John Roberts, akijibu ukosoaji mkali wa Donald Trump dhidi ya jaji wa shirikisho. Rais wa Mahakama ya Juu, mahakama ya juu zaidi nchini, alisisitiza kwamba utaratibu wa kukata rufaa “ulikuwepo kwa sababu hii,” na hivyo kukumbuka mfumo wa kitaasisi uliotolewa kwa kupinga uamuzi wa mahakama.

Mapema siku hiyo, Donald Trump alikuwa amemshambulia kwa jeuri James Boasberg, jaji wa shirikisho huko Washington, ambaye aliagiza siku ya Jumamosi, Machi 15, kusitishwa kwa agizo la kuwafukuza wahamiaji wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge kutoka Venezuela. Jaji huyo alikataa kuruhusu Ikulu ya Marekani kutegemea sheria ya wakati wa vita dhidi ya wageni ili kuhalalisha kufukuzwa kwao. Hata hivyo utawala wa Trump ulichukuwa njia yingine, ukiendelea kuwasafirisha wahamiaji hao katika nchi yao na kupuuza ombi la jaji la kurejesha ndege zinazobeba wahamiaji waliofukuzwa.

Mgawanyo wa madaraka

“Jaji huyu, kama majaji wengi wafisadi, ambaye ninalazimizimisha aweze kuripoti, anapaswa kuachishwa kazi,” bilionea huyo alidai kwenye jukwaa lake la Truth Social, akibaini kwamba alikuwa akifanya “kile tu wapiga kura walimuomba.” Jaji huyu “hakuchaguliwa kuwa rais,” amesisitiza, akimwita “mtu mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kushoto, mkorofi na mchochezi.” Wito uliosikilizwa na mwakilishi mteule wa chama cha Republican Brandon Gill, ambaye alitangaza kwenye X kwamba tayari amezindua utaratibu wa kumfungulia mashitaka mbele ya Baraza la Wawakilishi dhidi ya Jaji Boasberg, akielezwa kuwa “mwanaharakati mwenye msimamo mkali.”

Matamshi ya John Roberts yanaonyesha nia ya kutaka kuhifadhi uhuru wa mahakama wakati ambapo Donald Trump amekuwa akiwakosoa majaji wanaozuia sera zake. Uwezo wake wa kukataa kutii maamuzi ya mahakama, kama alivyofanya kwa kutaka kufutwa kazi kwa jaji – mara ya kwanza tangu kuanza kwa muhula wake mpya – hata hivyo kunazua hofu ya mgogoro wa kikatiba ambapo vyomvo vya sheria havitakuwa tena nguvu inayopingana na utawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *