WHO: Mfumo wa afya Gaza uko hatarini kusambaratika kabisa

Mwakilishi huyo wa WHO katika maeneo ya Palestina Rik Peeperkorn amesema uhaba wa mafuta pamoja na ukosefu wa mahitaji muhimu unauweka mfumo wa afya wa Gaza katika hatari ya kusambaratika.

Soma zaid: Israel yashambulia hospitali kaskazini mwa Gaza

Peeperkorn amefafanua kuwa ni hospitali 17 pekee kati ya 36 ndizo zinazotoa huduma kwa sasa, lakini pia ameelezea juu ya hali ngumu inayoikabili akisema, “Jana, Juni 16 kulikuwa na zaidi ya majeruhi 200 katika hospitali ya muda ya Shirika la msalaba mwekundu ya Al Mawasi na hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu waliopokelewa katika tukio moja. Zaidi ya wagonjwa 28 wameripotiwa kufa. Juni 15 hospitali hiyohiyo iliwapokea wagonjwa 170 waliokuwa  wakijaribu kulifikia eneo kunakotolewa msaada.”

Peeperkorn amesema bila mafuta kuingia Gaza watu watazidi kuteseka na kutakuwa na vifo vingi zaidi ambavyo vingeweza kuzuiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *