
Watu wasiopungua 59 wameuawa Gaza, wakati vifaru vya Israel viliposhambulia umati wa watu waliokuwa wakijaribu kupata msaada kutoka kwenye malori jana Jumanne.Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 60 Gaza
Mashahidi waliohojiwa na shirika la habari la Reuters, walisema vifaru vya Israel vilivyatua makombora mawili kwenye umati wa watu waliokuwa wamekusanyika kwenye barabara kuu ya mashariki kupitia Khan Younis kwa matumaini ya kupata chakula kutoka kwenye malori ya misaada yanayotumia njia hiyo.
Tukio hilo ni la karibuni zaidi katika mauaji ya karibu kila siku ya Wapalestina wanaokuwa wakitafuta msaada, katika muda wa wiki tatu tangu Israel iondoe kwa sehemu kizuizi katika eneo iliyokuwa imeweka kwa karibu miezi mitatu.
Israel imeruhusu misaada kuingia Gaza kupitia shirika jipya linaloungwa mkono na Marekani na Israel, ambalo linafanya usambazaji katika maeneo machache yanayolindwa na vikosi vya Israel.