
Huku mashambulizi kati ya Iran na Israel yakiendelea, dunia imepata hofu kuhusu hali ya usafirishaji wa mafuta na bidhaa utakavyokuwa katika bahari ya Arabia.
Hii ni kwa sababu, iwapo mapigano yataendelea, Iran inaweza kuamua kufunga njia kuu ya bahari inayoitwa Hormuz, ambayo ndiyo inayotumika kupitisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo mafuta ghafi, gesi na hata makontena.