Viongozi wa G7 wakamilisha majadiliano bila ya Trump

Viongozi wa kundi la nchi saba tajiri kiviwanda duniani G7, wamekuwa na siku ya mwisho ya majadiliano nchini Canada siku ya Jumanne, bila ya mshirika mkuu Rais Donald Trump wa Marekani. Trump alitangaza jumatatu jioni kuwa ataondoka mapema kutokana na mzozo wa Israel na Iran.

Mkutano huo wa kilele umezungumzia vita vinavyoendelea vya Urusi dhidi ya Ukraine, katika kikao kilichohudhuriwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Jumanne.

Zelensky, alikuwa amepanga kufanya mazungumzo ya pande mbili na Trump.Trump akatisha mkutano wa G7 wakati mzozo wa Israel na Iran ukiongezeka

Viongozi hao wa G7, wameshindwa kutoka na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo wa Ukraine baada ya Trump kuonyesha kumuunga mkono Rais wa Urusi Vladimir Putin. Trump aliweka wazi kuwa hatounga mkono, mpango wa pamoja wa kuiwekea vikwazo zaidi Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *