Ukraine: Mazungumzo mapya mjini London juu ya kusitisha mapigano, bila matumaini makubwa

Vita nchini Ukraine na njia za kufikia usitishaji vita na Urusi ni ajenda ya mkutano wa leo Jumatano, Aprili 23, nchini Uingereza. Wiki moja baada ya mkutano wa awali mjini Paris, wawakilishi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ukraine wanakutana mjini London. Mkutano huo, hata hivyo, haukuleta maendeleo yoyote makubwa. Inaonekana hakuna matumaini ya maendeleo madhubuti huko London.

Imechapishwa: 23/04/2025 – 05:35Imehaririwa: 23/04/2025 – 05:37

Dakika 2

Hii inafanana kama siku isiyokuwa na mwisho… Ukraine inasema iko tayari kwa usitishaji vita bila masharti, Urusi yapinga, mapigano yanaendelea, wakati Marekani inafikiriambinu zingine za kufanya. Leo Jumatano mjini London, mkuu mwenye ushawishi mkubwa wa utawala wa rais wa Ukraine, Andrii Yermak, atajaribu tena kuwafanya washauri wa Donald Trump kumshinikiza Vladimir Putin kufanya makubaliano.

Lakini hata kabla ya mkutano huu, Kremlin ilipunguza matumaini yoyote kuhusu mazungumzo ya amani. Siku ya Jumanne Urusi ilionya dhidi ya kuharakisha mazungumzo ya kusuluhisha mzozo nchini Ukraine, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema Jumapili kwamba anatumai makubaliano “ndani ya wiki moja” kati ya Moscow na Kyiv.

“Hili ni suala tata sana (…) kwamba pengine si bora kuweka makataa madhubuti na kujaribu kufikia suluhu ifaayo [ya mzozo] katika muda mfupi,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema katika mahojiano kwenye televisheni ya taifa ya Urusi.

Hakuna mawaziri wa ngazi ya juu wa Ufaransa au Marekani waliopo London

Wakati Donald Trump alikuwa bado anatumai makubaliano katika “siku zijazo” mwanzoni mwa juma, hayatakuwa hivi karibuni. Muundo wa wajumbe waliopo ni dalili. Hakuna waziri wa ngazi ya juu wa Ufaransa au Marekani atakayesafiri hadi London.

Steve Witkoff, mjumbe maalum wa Ikulu ya White House, anatarajiwa mjini Moscow. Itakuwa ziara yake ya nne nchini Urusi tangu kufufuliwa kwa uhusiano wa Urusi na Marekani ulioanzishwa katikati ya mwezi wa Februari na Donald Trump.

Marekani haijatumia “njia zote” ilizo nazo kuweka shinikizo kwa Urusi katika mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano nchini Ukraine, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas alisema katika mahojiano na shirika la habarila AFP siku ya Jumanne. Kulingana na mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Kyiv na wafuasi wake wa Ulaya walitumai kuwa Washington ingepitisha mstari mgumu zaidi kuelekea Moscow. “Wana mbinu mikononi mwao za kuweka shinikizo kwa Urusi. Kwa nini wasizitumie kumaliza vita hivi?” ameuliza. “Kama wanajiondoa sasa hivi bila kutumia mbinu  hizi (…) swali kubwa ni kwanini?” amesisitiza.

T

uko tayari kwa hatua hii. Pia tuko tayari kuthibitisha kwamba baada ya kusitishwa kwa mapigano, tutakuwa tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo, kwa namna yoyote ile. Ili kuepusha msuguano wowote wa aina “Ukraine inaweza kufanya hivi, haiwezi kufanya hivi, inataka hivi,” vyovyote itakavyokuwa. Kwa sababu katika hatua hiyo, tutazingatia kwamba tumepata angalau matokeo.

Post Views: 4