Timu ya Mlandege yatwaa ubingwa Ligi Kuu ZPL

By 
Zuleikha Fatawi

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Timu ya Mlandege imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar ZPL kwa msimu wa 2024-25 baada ya kuitandika New City mabao 4-2.

Mechi hiyo imehitimisha michezo 30 ya mzunguko wa ZPL na Mlandege, alitwaa ubingwa kwa idadi ya mabao 48,katika mchezo huu Abdallah Iddi aliipatia Mlandege bao la kwanza katika dakika ya 15, na bao la pili dakika ya 44.

Huku Said Khamis Matola akiipatia timu hiyo mabao mengine mawili kabla ya mchezo kumalizika na New City ikipata mabao mawili ya kufutia machozi dakika za jioni za mchezo huo.

Pia, Katika mchezo huo, Abdallah Iddi Pina ameibuka man of the Match katika mchezo huo.

Kwa upande mwengine, KVZ imechukua nafasi ya pili baada ya kuifunga timu ya Kipanga  bao 1-0 ikivuna alama 62 na kujipatia mabao 23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *