Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 16 zilizopita
Liverpool itajaribu kumshawishi kiungo wa kati wa England Adam Wharton, 21, kuondoka Crystal Palace kwa ada ya pauni milioni 50 na zaidi. (Sun)
Klabu ya Saudia Neom imeanza mazungumzo na wawakilishi wa mlinda lango wa Manchester United na Cameroon Andre Onana, 29. (Footmercato)
Mkufunzi wa Everton David Moyes anataka kumsajili kiungo wa kati wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 30, kutoka West Ham. (Sun)
Unaweza kusoma
Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 27, lakini hawako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Jarrod Bowen, 28. (Express)
Barcelona wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 25, kutoka Atletico Madrid kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 36. (Marca)
AC Milan wanafanya jitihada za kumbakisha kwa mkopo mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 27. (Gazzetta dello Sport )
Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim amemfanya mshambuliaji wa Nigeria mwenye thamani ya pauni milioni 40 Victor Osimhen, 26, kuwa mshambuliaji wake mkuu kwenye majira ya joto na Mashetani Wekundu wana nafasi nzuri ya kumnasa mchezaji huyu wa Napoli baada ya Chelsea kukataa uhamisho wake. (Mirror)
Winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 29, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na timu hiyo ya Bundesliga, na hivyo kumaliza matarajio ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kuhamia Arsenal au Liverpool. (Christian Falk via CF Bayern Insider)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Eric Ramsay yuko kwenye orodha ya Southampton ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu ajaye. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa zamani wa Wolves wa England chini ya umri wa miaka 21 Tommy Doyle, 23, anatazamiwa kuondoka msimu huu wa joto, na uhamisho wowote utanufaisha klabu ya zamani ya Manchester City, ambayo ina kipengele cha 50% cha mauzo. (Mirror)