Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 30 zilizopita
Arsenal wako katika hatua ya juu katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 26, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 60m (£51.2m) katika kandarasi yake. (ESPN)
Manchester United inaweza kumtoa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, kwa Atalanta badala ya mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27(Sun)
Roma, Napoli na vilabu viwili vyaligi ya Premea vina nia ya kumsajili winga wa Nottingham Forest wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 24, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wana nia ya kuamsha kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 30 katika mkataba wa mshambuliaji wa Ipswich na England wa Chini ya miaka 21 Liam Delap, 22, ambao utaanza kutumika ikiwa Tractor Boys watashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha, 25, yuko tayari kujiunga na Manchester United, ambao wamedhamiria kukamilisha dili la Mbrazili huyo msimu huu wa joto. (Sky Germany).
Tottenham Hotspur itaanza mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya beki wa Argentina Cristian Romero, 26, ambaye anafuatiliwa na Real Madrid na Atletico Madrid. (CaughtOffside)
Atletico Madrid pia wana nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham mwenye umri wa miaka 27 na Uruguay Rodrigo Bentancur. (Times)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 25, amepata majeraha manne akiwa kwa mkopo na Sevilla msimu huu na anatazamiwa kurejea Arsenal msimu wa joto, huku klabu hiyo ya La Liga ikiwa na uwezekano wa kutumia chaguo lao la £10.25m kumnunua. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hatacheza Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa mwezi Juni kwani hataki hatari ya kuumia na kuhatarisha utafutaji wake wa klabu mpya. (Daily Star)
Tottenham Hotspur wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, kwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Football transfer)
Wawakilishi wa mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr wanakanusha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Athletic)