Tanzania yapata zaidi ya dola milioni 110 kwa mauzo ya ufuta

Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya usimamizi wa mfumo wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu anasema hii ni kutokana na kuuzwa kwa tani 150,000 za ufuta nje ya nchi.

Tanzania inalenga kuimarisha kiwango hicho kwa kati ya tani 180,000 na 200,000 kwa mwaka 2025.

‘‘Katika msimu wa 2024, tuliuza tani 150,000 za ufuta nje ya nchi na kuingiza shilingi bilioni 300 (dola 113,640,000),’’ amesema Bangu.

Bangu alieleza kuwa vikao vya maandalizi vya mwaka huu vimehusisha wadau mbalimbali katika maeneo ambayo kunafanyika kilimo cha ufuta. Hasa wakilenga kuwapa elimu zaidi wakulima katika sehemu hizo.

Lengo la kuimarisha uuzaji nje ya nchi ni kuongeza pato la fedha za kigeni.

Katika mwaka 2024, Mataifa ya barani Afrika yaliyouza ufuta nje ya nchi ni pamoja na Nigeria (tani 357,000) na Sudan (tani 347,000). Tanzania ni ya tatu (tani 150,000). Mataifa mengine ni Ethiopia, Msumbiji na Chad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *