Raia kumi na sita wameuawa katika mji wa Aleppo katika shambulio linalodaiwa kutekekelezwa na Urusi, mshirika wa utawala wa Syria, limesema shirika la Haki za Bindamu nchini Syria (SOHR).

Matangazo ya kibiashara
“Watu wasiopungua 16 wameuawa na 20 kujeruhiwa wakati w ndege za kivita, pengine za Urusi, zilipolenga magari ya raia” katika sekta ya mji uliochukuliwa na waasi, limesema shirika la Haki za Binadamu nchini Syria, SOHR, ambalo lina mtandao mkubwa wa vyanzo nchini Syria.
Shirika hilo la Haki za Binaadamu la nchini Syria limesema shambulizi hilo lilipiga eneo la mji wa Aleppo ambao tayari unadhibitiwa na waasi.
Mapema, jeshi la Syria lilisema makumi ya wanajeshi wake wameuawa kaskazini mwa mji huo wa Aleppo na kuwafanya kurudi nyuma, hii ikiwa ni changamoto kubwa kwa Rais Bashar al Assad baada ya miaka mingi.
Wakati huo huo jeshi hilo lakini limesema linajiandaa kwa mashambulizi ya kushtukiza ili kuirejesha mamlaka.
Urusi ilianzisha mashambulizi ya anga katika sehemu za Aleppo usiku wa kuamkia Jumamosi kwa mara ya kwanza tangu 2016, waangalizi hao waliongeza.
SOHR ilisema zaidi ya watu 300 ikiwa ni pamoja na zaidi ya raia 20 wameuawa tangu mashambulizi kuanza siku ya Jumatano.