Rais wa Kenya William Ruto amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua nafasi ya mwenzake wa Sudani Kusini Salva Kiir. Ruto atashikilia wadhifa huo kwa mwaka mmoja ujao.

Matangazo ya kibiashara
Rais wa Kenya William Ruto, ameidhinishwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akimpokea mtangulizi wake Rais wa Sudani Kusini Salva Kirr.
Katika hotuba yake ya kukabidhi nafasi hiyo Rais Salva Kirr amesema ulikuwa ni wakati mzuri kwake kuhudumu katika nafasi hiyo na amaanini majadiliano ya kuijenga Jumuiya imara yataendelea chini ya Ruto.
Ruto ameidhinishwa katika mkutano wa 24 wa kilele wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo na atahudumu nafasi hiyo ya mzunguko kwa mwaka mmoja.
Mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unawaleta pamoja viongozi wa kanda hiyo ili kujadili masuala muhimu yanayochagiza mustakabali wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa hadhi ya juu, uliofanyika chini ya kaulimbiu kuu ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya EAC, unatumika kama jukwaa la kutathmini mafanikio ya miaka 25 iliyopita huku ukielekeza njia ya kusonga mbele kwa utangamano wa kina.
Mkutano huo pia umeidhinisha Kifaransa kuwa lugha rasmi, ikiifuatia lugha ya Kiswahili iliyoidhinishwa hivi karibuni