Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Papa Francis
Dakika 34 zilizopita
Papa Francis, mzaliwa wa Jorge Mario Bergoglio, ni mtu wa kwanza wa Amerika Kusini kuhudumu kama mkuu wa Kanisa Katoliki la Roma kwa miaka kumi na miwili. Alizaliwa huko Argentina.
1. Hakuzuru nchi yake wakati wa miaka 12 akiwa Papa.
Papa Francis hajawahi kutembelea nchi yake ya Argentina katika miaka 12 ya uongozi wake. Francis ametembelea nchi nne kati ya tano zinazopakana na Argentina.
Miezi mitatu baada ya kuwa mkuu wa kanisa, alifunga safari yake ya kwanza kwenda Brazil mnamo 2013.
Alikwenda Bolivia na Paraguay mwaka wa 2015, na Chile mwaka wa 2018. Pia alizuru katika baadhi ya nchi za Amerika Kusini kama vile Cuba, Ecuador, Mexico na Peru.
Hatahivyo, swali la kwanini hakurudi nyumbani limekuwa swali ambalo limekuwa likiulizwa kila wakati. Hii inadhihirisha uhusiano mgumu wa Papa Francis na nchi yake.
Ingawa kuna watu wengi wanaovutiwa naye, wengi wanamkumbuka kama mtu mwenye utata.
Papa Francis amekuwa akitoa majibu yasiyoeleweka kila mara anapoulizwa kuhusu safari yake ya Argentina.
“Nataka kwenda. Ni watu wangu. Lakini bado sijapanga. Kuna mambo mengi ya kusuluhishwa kabla ya hapo,” alisema mnamo Septemba 2024.
Papa Francis hataki safari yake itumike kwa madhumuni ya kisiasa, alisema msaidizi wake wa karibu Gustavo Vieira.
Vera alisema kuwa Papa alikuwa akifahamu kila mara kile kinachotokea nchini Argentina na alijadili kila kitu.
Vieira alisema angeenda Argentina tu wakati anahisi anaweza kuwa chombo cha kuleta umoja wa kitaifa na kuwaunganisha Waajentina.
Chanzo cha picha, Getty Images
Pia unaweza kusoma
2. Aliwahi kuwa mlinzi wa klabu ya usiku {bouncer}
Bergoglio alikulia Buenos Aires, mji mkuu wa Argentina, na alimaliza elimu yake ya sekondari na kujipatia diploma yake katika somo la kemia
Baada ya kupata shahada ya theolojia (somo la imani za kidini), aliendelea kufundisha fasihi na saikolojia.
Katika mahojiano aliyofanyiwa mwaka wa 2010, alisema kwamba babake alimshinikiza apate kazi akiwa na umri wa miaka 13 na hata akapanga afanye kazi katika kiwanda cha nguo.
Miaka michache baadaye, akizungumza katika kanisa moja huko Roma, alisema kwamba alikuwa amefagia sakafu na kufanya kazi ya kuweka usalama katika klabu ya usiku.
Alisema pia alifanya kazi katika kiwanda cha kusindika chakula.
Chanzo cha picha, Getty Images
3. Ni shabiki mkubwa wa soka
Papa Francis ni shabiki mkubwa wa klabu ya soka ya San Lorenzo de Almagro, ambayo ilishinda Copa Libertadores, shindano la kifahari zaidi katika kandanda ya vilabu vya Amerika Kusini, kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 106.
Alipoulizwa, “Je, ushindi huu unatokana na msaada wako?” alisema, “Nina furaha sana. Lakini ushindi huu sio muujiza.”
Papa Francis amekutana na magwiji wengi wa soka.
Mechi nne kati ya za ngazi ya juu za soka ya Italia zilizopangwa kufanyika Jumatatu ya Pasaka ziliahirishwa kufuatia kifo cha Francis.
Chanzo cha picha, Getty Images
4. Anapenda usafiri wa basi
Papa anapenda maisha rahisi. Hata gari analosafiria linaonyesha maisha yake rahisi.
Baada ya kuchaguliwa kuwa Papa, alipanda basi moja kwa moja na makadinali wake. Papa Francis ameweka wazi kuwa anapendelea magari ya kawaida kuliko magari ya kifahari.
Kabla ya kuwa papa, mara nyingi alisafiri kwa mabasi na treni za chini ya ardhi za jiji. Alipokuwa akisafiri kwenda Vatikan, alisafiri kwa kutumia treni ya tabaka la chini.
Siku moja kabla ya kifo chake, alikwenda kwenye Uwanja wa St. Peter’s Square, akiwapungia mkono na kuwasalimia watu akiwa kwenye gari la ‘Pope Mobile’ lililokuwa mgongo wazi.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Papa Francis akipeana mkono na mtangazaji wa Runinga wa Marekani Jimmy Fallon alipokutana na wacheshi zaidi ya 100 mjini Vatican mwezi Juni 2024
5. Ni mcheshi
Papa Francis anajulikana sana kwa kuwa mcheshi, pamoja na hoja zake na kejeli.
Mwaka jana (2024), programu iliandaliwa kwa kuwaalika zaidi ya wacheshi mia moja kutoka nchi 15 hadi Vatikan.
Papa Francis aliwaambia kwamba amekuwa akiomba kila siku kwa zaidi ya miaka 40, “Mungu, nipe ucheshi mzuri.”
Thomas More, ambaye alifungwa gerezani katika karne ya 16, pia alisali sala hiyo. Baadaye akawa mtakatifu wa Kanisa Katoliki.
Chanzo cha picha, Getty Images
6. Ana ufuasi mkubwa mtandaoni
Papa Francis alisema mwaka wa 2018 kwamba ‘mtandao ni zawadi kutoka kwa Mungu.’ Alisema kuusimamia ni jukumu kubwa.
Papa Benedict XVI, ambaye alihudumu kabla ya Papa Francis, alifungua akaunti kwenye jukwaa la wakati huo la Twitter (sasa Ex) mwaka wa 2012. Hata hivyo, akaunti hiyo ilipata wafuasi wengi baada ya Francis kuwa Papa.
Papa alikuwa akichapisha maudhui yake kwa lugha tisa na alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 50.
Akaunti ya Papa ya Instagram ina wafuasi milioni 9.9. Amesema kuwa teknolojia mpya haziwezi kuchukua nafasi ya mahusiano ya kibinadamu.
Kabla ya kifo chake, pia alichapisha ujumbe wake kwenye X siku ya Jumapili ya Pasaka.
Pia unaweza kusoma
Imetafsiriwa na Seif Abdalla