Ndugu Magambo Nkama Samwel ni Mjiolojia mwenye elimu ya juu kutoka nchini Uingereza, alikopata Shahada ya Kwanza na Shahada ya U…

Ndugu Magambo Nkama Samwel ni Mjiolojia mwenye elimu ya juu kutoka nchini Uingereza, alikopata Shahada ya Kwanza na Shahada ya U…

Ndugu Magambo Nkama Samwel ni Mjiolojia mwenye elimu ya juu kutoka nchini Uingereza, alikopata Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) katika fani ya Jiolojia. Alitunukiwa Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Aberdeen mwaka 2020, akibobea katika utafiti na uzalishaji wa madini, mafuta, gesi asilia na maji.

Kwa zaidi ya miaka 11, amehudumu ndani ya Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), akiwa sehemu ya timu ya kitaifa ya wataalamu waliotekeleza miradi mikubwa ya mafuta na gesi kwa kushirikiana na makampuni ya kimataifa. Magambo ameshiriki moja kwa moja kwenye tafiti zilizogundua gesi asilia inayotumika hivi sasa kuzalisha zaidi ya 60% ya umeme nchini.

Kisiasa, Magambo ni kada mwaminifu wa CCM tangu mwaka 2010. Ameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa chama kuanzia ngazi ya matawi hadi wilaya, na amekuwa sehemu ya juhudi za kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, hasa katika Jimbo la Kishapu.Mara kadhaa amewezesha chama na jumuiya zake katika mikutano, warsha na vikao vya kimkakati vya maendeleo.

Kwa jitihada zake, amefanikisha uletwaji wa mradi wa utafiti wa mafuta na gesi katika bonde la Eyasi Wembere linalopita kata za Shagihilu, Masanga na Mwamalasa ndani ya Wilaya ya Kishapu. Mradi huu tayari umefungua ajira kwa vijana na kina mama, na matarajio ya kugundulika kwa rasilimali hizo yanatarajiwa kuifanya Kishapu kuwa kitovu cha uchumi na maendeleo ya nishati ya uhakika nchini.

Magambo amejipanga kuwapigania Wananchi kuhakikisha wanapata maendeleo kwenye Sekta ya kilimo ambayo ni ajenda yake kuu kwa kutambua kwamba zaidi ya 86% ya Wananchi wa kishapu ni wakulima na wafugaji kwa kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija na kuhakikisha kilimo kinakuwa ni ajira kwa vijana na kunaleta ujenzi wa viwanda vikubwa na vidogo
Ndugu Magambo pia kama Sauti ya wanakishapu amejipanga kuwainua wananchi kiuchumi kupitia Madini yanayopatikana katika wilaya ya Kishapu hasa madini ya Almasi kwa kuhakikisha wanapata maeneo yaliyofanyiwa utafiti wa kina wa upatikanaji wa madini hayo, Magambo kama Mwakilishi atahakikisha kukomesha matumizi ya nishati chafu kama kuni na mkaa na badala yake watumie Gesi asilia ambayo pia inaweza kupatikana kutokana na utafiti wa gesi asilia na mafuta unaoendelea kufanywa na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) katika kata za Masanga, Shagihilu na Somagedi Wilayani KISHAPU na pia atahakikisha Wananchi wa Kishapu wanapata maji kila kaya kutokana na uwepo wa Bomba la ziwa Victoria pamoja, gridi ya Taifa ya Maji na uchimbaji wa visima vya maji kama ulivyoainishwa kwenye ilani ya chama cha Mapinduzi ya 2025/2030.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *