Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka linapaza sauti baada ya mmoja wa wafanyakazi wake kuuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake jioni ya Aprili 18 mashariki mwa DRC. Muuguzi katika Hospitali Kuu ya Masisi, ni mfanyakazi wa pili wa MSF kupigwa risasi katikati ya Masisi chini ya miezi miwili. Pia ni mfanyakazi wa tatu wa MSF kupoteza maisha kwa kupigwa risasi tangu mwanzoni mwa mwaka katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Imechapishwa: 25/04/2025 – 07:39
Dakika 2
Mfanyakazi wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) aliuawa kwa kupigwa risasi Aprili 18 mashariki mwa DRC “na mtu aliyekuwa na silaha,” shirika hilo lisilo la kiserikali lmeisema katika taarifa siku ya Alhamisi, Aprili 24, likiwataka wanamgambo na wanajeshi wa Kongo “kukomesha ghasia dhidi ya raia na wafanyakazi wanaojitolewa kusaidia raia kutoka mashirika ya kihisani.” Mwishoni mwa mwezi wa Februari, mfanyakazi mwingine wa shirika hilo la kibinadamu alifariki baada ya kujeruhiwa vibaya na risasi wakati wa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya kundi la waasi la M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali. Matukio yote mawili yalitokea Masisi, mji wa mkoa wa Kivu Kaskazini.
Mashariki mwa DRC, eneo tajiri wa maliasili na linalopakana na Rwanda, limekuwa likikumbwa na migogoro kwa miaka thelathini. Ghasia zimeongezeka katika miezi ya hivi majuzi baada ya miji mikuu ya Goma na Bukavu kudhibitiwa na kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Kigali.
Mfanyakazi wa MSF ‘aliuawa’
“Siku ya Ijumaa, Aprili 18, wanaume wawili waliovalia sare za kijeshi wakiwa na bunduki za kivita waliwashambulia na kuwanyang’anya mali zao raia katika mji wa Masisi kabla ya kuvunja nyumba ya mfanyakazi wa MSF ili kupora mali zake,” MSF imesema, bila kutaja jina la mwathiriwa. “Watu hawa wenye silaha walitumia silaha zao, na kumjeruhi vibaya mfanyakazi wa MSF, ambaye alipigwa risasi mbili kifuani,” limeongeza shirika hilo, ambalo limerekodi takriban matukio kumi na tano tangu mwezi wa Januari yakiathiri timu zake au mashirika yanayouliunga mkono.
Akinukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwakilishi wa MSF nchini DRC, Emmanuel Lampaert, anazungumzia majanga yasiyokubalika ambayo hayapaswi kurudiwa.
Hii inaonyesha kuzorota kwa ujumla kwa hali ya usalama.
“Hata mbali na mstari wa mbele, ukosefu wa usalama upo kila mahali,” ameonya Mathilde Guého, mkuu wa programu za MSF huko Kivu Kaskazini. MSF ina takriban wafanyakazi 3,000 wa ndani na nje ya nchi nchini DRC.
Post Views: 2