Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa jeshi hilo linatoa nafasi kwa vijana wa kidato cha sita wanaojiunga na jeshi hilo kutuma maombi ya vyuo pale muda utakapofika ikiwemo kuwarudishia simu vijana hao ili waweze kuwasiliana na wazazi na kushauriana ziadi.
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo katika kipindi cha #DAKIKA45 na kwamba amefanya hivyo baada ya kubaini changamoto hiyo katika kipindi cha nyuma.