Mwanariadha wa Kenya Emmanuel Wanyonyi amekuwa na matokeo bora zaidi katika msururu wa mbio za Stockholm Diamond League, kwa kushinda mbio za mita 800 kwa wanaume katika muda wa dakika 1 sekunde 41.95.
Muda huu wa Wanyonyi ndiyo bora zaidi katika mbio hizo kufikia sasa mwaka huu, na pia ni ushindi wake wa pili katika mfululizo wa mbio za Diamond League.
Matokeo hayo yamedhihirisha mafanikio ya wanariadha wa Kenya katika mbio za masafa ya kati.
Msimu wa riadha sasa unaendelea kukiwa na mbio mbalimbali zilizopangwa kufanyika katika maeneo tofauti.
Kwa sasa wanariadha kama Wanyonyi na wengine wa Kenya wanajitahidi kuendeleza matokeo mazuri, huku wakiangazia mashindano ya mbio za dunia yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba jijini Tokyo, Japan.