#MICHEZO: Mashindano maalum ya mchezo wa soka, yaliyohusisha timu 22 kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma, uliopo wilayani Momba…

#MICHEZO: Mashindano maalum ya mchezo wa soka, yaliyohusisha timu 22 kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma, uliopo wilayani Momba…

#MICHEZO: Mashindano maalum ya mchezo wa soka, yaliyohusisha timu 22 kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma, uliopo wilayani Momba, mkoani Songwe, yaliyolenga kuhamasisha amani kuelekea Uchanguzi Mkuu, unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, yametamatika huku timu ya Tunduma City, wakiibuka mabingwa na kujinyakulia zawadi ya kombe na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja, huku timu wakishiri wakiondoka na zawadi mbalimbali ikiwemo mipira.

Muandaaji wa mashindano hayo yanayojulikana kama Tom Super Cup, Bw. Thom Mkondya, amesema mbali na kulenga kuibua na kuendeleza vipaji shabaha nyingine ni kuhakikisha mji wa Tunduma, una kuwa na amani hasa kwa vijana ambao wamekuwa wakitumika na bila kujitambua nakuwa waathirika wakubwa pindi zinapotokea vurugu.

Aidha ameongeza kuwa matamanio yake ni kuona Mji wa Tunduma na Mkoa wa Songwe, kiujumla unainuka kimichezo ikiwemo soka kwa kuendelea kudhamini timu na mashindano mbalimbali huku Uongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Momba, kupitia kwa Katibu wake Bw. Edward Mbambali wakipongeza jitihada za mdau huyo.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *