“Mheshimiwa Spika, naomba kusisitiza kuwa, sisi viongozi tuwe mstari wa mbele katika kulipa kodi, kuwahamasisha wananchi kulipa kodi stahiki kwa hiyari pamoja na kuhakikisha hatutumii mamlaka na madaraka yetu kusaidia ukwepaji kodi, ikumbukwe hata Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “Kila Mtanzania anapaswa kuelewa kwamba maendeleo hayawezi kupatikana kwa kutegemea misaada, ni lazima tulipe kodi,”- Dkt Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha akisoma Bajeti Kuu ya Serikali 2025-26 bungeni jijini Dodoma.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania