“Mheshimiwa Spika, jumla ya kilometa 52.5 za barabara za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zimejengwa kwa kiwa…

“Mheshimiwa Spika, jumla ya kilometa 52.5 za barabara za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zimejengwa kwa kiwango cha lami. Barabara zilizokamilika ni pamoja na:
i. Barabara ya Kimara – Kibaha (19.2)
ii. Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya II kutoka Maktaba – Mbagala (km 19.3)
iii. Barabara ya Ardhi – Makongo (km 4)
iv. Barabara ya Wazo Hill – Madale (km 9).
v. Daraja la Tanzanite (km 1.03).
vi. Madaraja ya juu ya Chang’ombe na Uhasibu. Vilevile, miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na:
i. Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya III kutoka Maktaba – JNIA – Gongolamboto (km 23.3);
ii. Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya IV kutoka Maktaba – Morocco – Mwenge – Tegeta na Mwenge -Ubungo (km 30.1); na
iii. Maandalizi ya kuanza ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya V kutoka Ubungo – Bandarini, Makutano ya Tabata –Tabata Segerea na Tabata – Kigogo (km 27.6),” – Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *