Mawakili wa Uganda Wapinga Mahakama za Kijeshi kwa Raia

Muswaada wa sheria hiyo ni mingoni mwa ile ambayo imewahi kupitishwa kwa haraka bungeni huku kukiwa na madai kwamba wabunge wa chama tawala NRM na wale huru wanaoegemea chama hicho walipokea kiasi cha shilingi milioni 100 miezi miwili iliyopita kupitisha muswaada huo uliofanyiwa marekebisho kufuatia maamuzi na ushauri wa mahakama ya juu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo iliyotiwa saini na rais Museveni jana alasiri, raia yeyote atayekamatwa akiwa na silaha na mavazi yanayoshabihiana nay a kijeshi atafunguliwa mashtaka katika mahakama hiyo.

Mara kadhaa wafuasi wa upinzani hasa wale wa chama kikuu cha upinzani cha NUP kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi wamekuwa wakikamatwa kwa kuvalia bwelasuti ( overall) na kofia za bereti.

Hali hii ndiyo inawapelekea wengi wao kuhisi kwamba sheria hiyo imelenga kukandamiza upinzani hasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu Nicholas Opiyo ametoa angalizo kuwa hila ya spika wa bunge kushinikiza kupitishwa haraka kwa muswaada husika pamoja na tamko la rais Museveni akimpongeza kufanya hivyo ni kielelezo dhahiri kwamba sheria hiyo itakuwa muhimu sana katika kukandamiza upinzani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Wasiwasi wa upinzani na wanaharakati

Polisi Uganda wamelaumiwa kuwanyanyasa wapinzani na wanaharakati
Polisi Uganda wamelaumiwa kuwanyanyasa wapinzani na wanaharakatiPicha: Badru Katumba/AFP/Getty Images

Mashaka mengine ni kwamba huenda mwanasiasa Dkt Kiza Besigye ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Museveni atarudishwa katika mahakama ya jeshi kuhusiana na kesi ya uhaini na kupatikana na silaha.

Tangu alipokamatwa mwezi Novemba mjini Nairobi, Dkt Besigye amebaki gerezani hata baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali uhalali wa ile ya jeshi ambayo ilikuwa ikiendesha kesi dhidi yake. Wadadisi wa siasa za Uganda wanaongezea hivi.

Jumuiya ya wanasheria na wapiganiaji mbalimbali wa hakiza binadamju wameapa lkuwasilisha shauri katika mahakama ya katiba kupinga utekelezaji wa sheria hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *