Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza siku ya Jumapili kwamba amemsamehe mtoto wake Hunter, ambaye alikuwa akisubiri kuhukumiwa katika kesi za kumiliki silaha kinyume cha sheria na kukwepa kulipa kodi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Hakuna mtu mwenye busara anayeangalia ukweli katika kesi za Hunter anayeweza kufikia hitimisho lolote isipokuwa hili: Hunter alitengwa kwa sababu tu ni mtoto wangu – na hiyo sio sawa,” Rais Joe Biden amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, akimaanisha ” kosa la kimahakama”. Hata hivyo Kiongozi huyo wa Marekani alihakikisha mara kadhaa kwamba hatatoa msamaha wa rais kwa mwanawe. Hivi majuzi mnamo mwezi wa Septemba, Ikulu ya White House ilithibitisha hili.
Hunter Biden, 54, alikiri hatia mnamo mwezi wa Septemba ya kukwepa kulipa kod katika mahakama ya Los Angeles, California, na hivyo kuepuka kesi. Mwanasheria huyu wa zamani na mfanyabiashara, ambaye sasa amebadilishwa katika uchoraji, alikabiliwa haswa na shtaka moja la ukwepaji kodi na makosa mawili ya matamko ya uwongo kwa kutolipa kodi wa dola milioni 1.4 katika muongo mmoja uliopita. Mtoto wa mwisho wa Joe Biden tayari amepatikana na hatia mwaka huu kwa kusema uwongo kuhusu uraibu wake wa dawa za kulevya wakati akinunua silaha – jambo ambalo ni kosa katika jimbo la Delaware, ngome ya Biden. Hunter Biden alikuwa bado anangoja kujua ni hukumu gani atapokea katika kila moja ya kesi hizi.
“Nilisema sitaingilia maamuzi ya Wizara ya Sheria na nilitimiza ahadi yangu hata nilipoona mwanangu akifunguliwa mashtaka kwa njia isiyo ya haki,” Joe Biden amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. “Mashtaka katika kesi zake yaliibuka tu baada ya wapinzani wangu kadhaa wa kisiasa katika Bunge la Congress kuwachochea kunishambulia na kupinga kuchaguliwa kwangu,” ameongeza. “Ninaamini katika mfumo wa haki, lakini […] Pia ninaamini [kwamba] aina ya siasa chafu imeambukiza mchakato huu na [kwamba] hii imesababisha kukosekana kwa haki.