MAKANISA SITA YA UFUFUO NA UZIMA MBEYA YAFUNGWA
#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Limeyafungia makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa Wilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe na Kyela.
Hii ni kufuatia tamko la Serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia Msajili wa Jumuiya za Kiraia Nchini la kufunga Makanisa ya Ufufuo na Uzima kwa kutoendelea kutoa huduma katika Matawi yake yote yaliyopo nchi nzima.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Benjamin Kuzaga amesema wanaendelea ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa Makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria na mpaka sasa wameweka ulinzi ili huduma zisiendelee.
#itvdigital #itvupdates #itvtanzania.
#follow @radioonetanzania