“Kuhusu Wakandarasi wa Ndani, ambao wanatekeleza zaidi ya asilimia 70 ya kazi za Sekta ya Maji, napenda kuwambia, Wizara itaendelea kuwaamini na kuwajengea uwezo ili mzidi kukua. Ninawashukuru sana kwa kuwa ushirikiano tulionao unadhihirisha ukweli kuwa; figa moja haliinjiki chungu”; kidole kimoja hakivunji chawa”; na “uliyeokota naye kuni ndiye wa kuota naye moto”. Tumevuja jasho pamoja na Wakandarasi, Wataalamu Washauri na Watoa Huduma; tuidumishe timu yetu ya ushindi, tufurahie mafanikio pamoja”-Mhe. Jumaa Aweso Waziri wa Maji.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania