Chanzo cha picha, EPA
Dakika 26 zilizopita
Kila wakati Papa Francis alirudi Roma baada ya safari ya nje ya nchi, alihakikisha anatembelea kanisa la Santa Maria Maggiore.
Lilikuwa chaguo lifaalo: Francis alijitolea hasa kwa Bikira Maria, na Santa Maria Maggiore lilikuwa kanisa la kwanza kuwekwa wakfu lilipojengwa katika Karne ya 4.
Ni moja ya basilica nne kuu za Roma na moja ya kongwe zaidi katika jiji hilo.
Siku ya Jumamosi, itakuwa pia mahali pa kupumzika pa mwisho pa Francis.
Ni umbali mfupi kutoka kwa baadhi ya alama muhimu za Roma kama vile Colosseum, na kutoka kituo cha katikati cha Termini chenye shughuli nyingi. Kitongoji tofauti cha Esquilino kiko karibu.
Santa Maria Maggiore ni kama Roma “halisi” – licha ya kiufundi kuwa sehemu ya jimbo la Vatican.
Una vituo vya mabasi, mikahawa na maduka, kwa hakika inaonekana kuwa ulimwengu ulio mbali na Uwanja wa St Peter’s Square unaostaajabisha na kanisa lake la kuvutia, ambalo Mapapa huzikwa chini yake kwa mapango ya karne nyingi.
Makanisa, michoro na mbao zilizopambwa za Santa Maria Maggiore zinabaki kuwa za kushangaza. Mapapa wengine saba wamezikwa hapa.
Basilica hiyo pia ni mwenyeji wa kile kinachosemekana kuwa mabaki ya kitanda cha Yesu na sanamu ya Mariamu, ambaye Papa Francis alisali kuomba ulinzi kabla ya safari.
Chanzo cha picha, Reuters
Kasisi mkuu wa Santa Maria Maggiore, Mlithuania Rolandas Makrickas, alilipatia gazeti la Italia Il Messaggero maelezo yake kuhusu jinsi uamuzi wa Papa kuzikwa hapo ulivyotokea.
Alisema: “Mnamo Mei 2022… nilimuuliza ikiwa hakuwa na bahati yoyote kufikiria kuhusu kuzikwa katika [basilika], ikizingatiwa ni mara ngapi alifika.”
Francis alitabasamu na kusema kwamba Mapapa wamezikwa huko St Peter’s , “na hiyo ilikuwa hivyo”, Matrickas alifikiria.
Kasisi huyo aliendelea: “Wiki moja baadaye aliniita na kusema, ‘Bikira Maria ameniambia nitayarishe kaburi langu’.
“Kisha aliniambia kwa urahisi, ‘tafuta mahali kwa ajili hiyo, kwa sababu ninataka kuzikwa katika kanisa hili na umekuwa nabii kidogo’.”
Mahali ambapo Macrickas alipata ni karibu na sanamu ya Mariamu ambayo Papa aliipenda sana. Sasa imefungwa na kufunikwa na ‘plywood’.
Mlinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia BBC habari za Papa Francis kuzuru kanisa hilo mara nyingi.
“Baada ya kumuona mara kadhaa, wakati mmoja alinitazama na kuniuliza, ‘mbona uko hapa kila wakati?’
“Nami nikasema, ‘Baba Mtakatifu, ninafanya kazi kama wewe.
Chanzo cha picha, Reuters
Wakati mlinzi huyo akiongea, watu waliendelea kumiminika kutoka kwenye jua kali hadi kwenye kivuli tulivu cha basilica.
Watu kadhaa walipanga foleni nje ya vibanda vya mbao, kila kimoja kikiwa na ishara inayoonesha lugha ambazo makasisi waliokuwa ndani wangeweza kusikia maungamo.
Kila baada ya dakika chache, gumzo lilinyamazishwa kwa muda kupitia kipaza sauti: “Silenzio.” (Kimyaa!)
Huku nje, mwanamke anayeitwa Pat kutoka Manchester alikuwa akikodolea macho jua akiwa mwenye mawazo.
“Nilikuja hapa kwa sababu hapa ndipo Papa alikuwa akija kabla ya safari yoyote,” aliiambia BBC, akipaza sauti yake kutokana na mlio wa kengele za mchana.
“Ndio maana siku zote nimekuwa nikitaka kuja na haijakatisha tamaa.”
Chanzo cha picha, Reuters
Pat alisikia habari kuhusu kifo cha Papa wakati ndege yake kutoka Uingereza ilipotua Roma Jumatatu asubuhi.
Haikukatisha tamaa ziara yake. Kama Mkatoliki mwaminifu, alisema Santa Maria Maggiore “siku zote palikuwa mahali nilipotaka kuja” kwa sababu Francis alipapenda sana.
Jumamosi mchana, baada ya ulimwengu kupata nafasi ya kumuaga, Papa Francis atafunga safari yake ya mwisho kutoka Vatican hadi Santa Maria Maggiore, kama alivyokuwa akifanya mara nyingi maishani.
Kanisa lilifungwa kwa saa chache, kisha wageni waliendelea tena.
Wengine, kama Pat, waliendelea kuja basilica. Wengine walivutiwa tu na michoro.