Jeshi la Urusi limetangaza siku ya Ijumaa Novemba 29, 2024 kwamba limetungua ndege 47 zisizo na rubani za Ukraine usiku ambazo zililenga zaidi eneo la Rostov, linalopakana na Ukraine, ambapo moto mkubwa ulizuka kwenye eneo la viwanda. “Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imeharibu ndege zisizo na rubani 47 za Ukraine,” zikiwemo ndege 29 katika eneo la Rostov (kusini) ambalo ni makao makuu ya operesheni ya Urusi nchini Ukraine, jeshi limesema katika taarifa.
Matangazo ya kibiashara
Katika mkoa wa Rostov, moto mkubwa umezuka kwenye “eneo la viwanda” katika wilaya ya Kamensky, na zaidi ya wazima moto mia moja wametumwa huko, kulingana na gavana wa eneo hilo Yuri Sliosuar ambaye ameripoti kwenye Telegraph “shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani” ambalo limelenga mkoa wake. Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, shambulio hilo limesababisha moto katika ghala la mafuta karibu na Kamensk-Shakhtinsky.
Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Beloussov amewasili siku ya Ijumaa Novemba 29 nchini Korea Kaskazini kwa ziara ya kiserikali, jeshi la Urusi limetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari. Wakati wa “ziara rasmi” huko Pyongyang, mshirika wa Moscow, Belooussov atakutana na baadhi ya “maafisa wa kijeshi na viongozi wa kijeshi na kisiasa” wa Korea Kaskazini, jeshi la Urusi limebainisha, bila maelezo zaidi.
Urusi na Korea Kaskazini zinaungana kwa mkataba wa ulinzi wa pande zote, uliotiwa saini mwezi Juni na kuidhinishwa hivi majuzi. Seoul na Washington zinaishutumu Korea Kaskazini kwa kutuma wanajeshi nchini Urusi kusaidia wanajeshi wa Urusi kupigana, dhidi ya vikosi vya Ukraine, Seoul na Washington wanasema.